SEAT OF WISDOM PRE & PRIMARY SCHOOL

SEAT OF WISDOM PRE AND PRIMARY SCHOOL

ENGLISH MEDIUM

 

Shule hii ipo Mkoa wa Kigoma, Wilaya ya Kasulu, ndani ya halmashauri ya mji Kasulu, kata ya Murusi , mta wa Kwizera barabara ya kuelekea Kibondo kilipokuwa Chuo cha ufundi KTS . Shule yetu hii mpya itakapokamilika kujengwa itakuwa ni shule ya kuanzia elimu ya awali, msingi na sekondari na itafundisha masomo yote kwa ngazi husika na itakuwa ni shule ya mchepuo wa UFUNDI.

Kwa kuzingatia hitaji kubwa la shule za namna hii katika mji wetu wa Kasulu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla, na kwa kuzingatia mfumo mpya wa elimu wa Tanzania na kwa kuzingatia mahitahji ya Ulimwengu huu wa sasa wa Sayansi na Teknolojia, Mhashamu Baba Askofu Joseph R. Mlola, ALCP/OSS  wa Jimbo Katoliki  Kigoma ameamua kuanzisha shule hii mpya inayochukua wanafunzi wa DINI ZOTE itakayokuwa ya kisasa sana na itakayokidhi mahitaji ya sasa na baadae ya jamii yetu.

Baba Askofu ameamua kuanzisha shule hii ya kwanza na ya kipekee katika mji wa Kasulu na mkoa wa Kigoma ili kuanza kuwaandaa watoto wakiwa bado wadogo waweze kupata maarifa mbalimbali ya ufundi na hivyo baadae waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za ajira zinazoikabili nchi yetu na ulimwengu mzima. Tunasema shule hii ni ya kipekee kwa sababu ndiyo shule ya kwanza mkoani Kigoma ambayo itakuwa na michepuo ya ufundi kuanzia shule ya msingi hadi sekondari katika eneo moja.

Shule hii ipo katika mazingira bora, ina huduma bora za chakula cha asubuhi na mchana kwa watoto, huduma za uhakika za umeme na maji na inasimamiwa na WATAWA ( Masista ) waliobobea katika kusimamia taaluma na malezi ya watoto na hivyo mtoto wako akisoma katika shule  hii atapata malezi bora ya maadili ya Kitanzania na hivyo kumwandaa kuja kuwa mtaalamu mbobevu katika fani mbalimbali na mwenye maadili yasiyo tiliwa shaka.

Karibu sana shuleni kwetu,

 

S.L.P 123 KASULU-KIGOMA

Kibondo Road; Simu: 0769946954;   0768439116 ;    0762998056 :

E -mail : seatofwisdom@kigomadiocese.org